Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Radhavi Mehr, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza na Wanazuoni wa Hawza ya Qom, pamoja na baadhi ya viongozi wa baraza hilo, walikutana na kufanya mazungumzo na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Farrokh-Fal, Msimamizi wa Sekretarieti ya Baraza Kuu la Hawza.
Msimamizi wa Sekretarieti ya Baraza Kuu la Hawza alilitaja Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza kuwa ni amana ya Imam Khomeini (ra), na akasema: “Imam Khomeini na Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi (ra) walikuwa wakilipa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza thamani kubwa.”
Akirejelea uwezo mkubwa na huduma zilizotolewa na Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza hapo nyuma, alisema: “Viongozi wakuu wa Hawza watatoa uangalizi unaostahili kwa baraza hili. Baraza hili lina ufanisi mkubwa sana, baraza la Wawakilishi lina athari na baraka nyingi katika Hawza, na miongoni mwa huduma zake ni pendekezo la kuanzishwa Kituo cha Huduma, ambacho hivi sasa ni mhimili madhubuti wa kuwaunga mkono wanafunzi wa Hawza na wanazuoni.”
Msimamizi wa Sekretarieti ya Baraza Kuu la Hawza alielezea uanzishaji wa mawasiliano kati ya wanafunzi wa Hawza na taasisi za juu za Hawza kupitia baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza kuwa ni sababu ya mafanikio ya Hawza, na akaendelea kusema: "Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi wa Hawza ni jukwaa na uwezo muhimu ambao Imam Shahidi, katika suala la kubaki Hawza kuwa ya kimapinduzi, alielekezea mkazo. Na ikiwa tunataka Hawza itekeleze majukumu yake ya msingi, baraza la wawakilishi linapaswa kutekeleza nafasi yake kama kiungo kati ya Baraza Kuu na Jumuiya ya Walimu wa Hawza, kwa upande mmoja, na jumuiya ya wanafunzi wa Hawza kwa upande mwingine.”
Hujjatul-Islam wal-Muslimin Farrokh-Fal, akizungumzia hali ya nchi ya Iran, alisema: “Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu, tutamfanya adui ajutie kupitia muqawama wetu madhubuti, na tunatumaini kwamba katika siku zijazo wapiganaji wetu wataweza kumshambulia adui kwa mashambulizi ya mwisho ya kuamua; lakini kwa sasa tunapaswa kuwa na subira na uvumilivu kuhusu kuwepo kwa baadhi ya matatizo.”
Mjumbe wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qom alieleza matumaini yake kwamba: “Matatizo na changamoto zinazolikabili baraza la wawakilishi wa wanafunzi na wanazuoni wa hawza ya Qom katika kutekeleza jukumu lake na kutoa huduma zaidi kwa wanafunzi wa Hawza na wanazuoni, zitaondolewa katika siku zijazo.”
Mwanzoni mwa mkutano huu, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Jalal Ridhavi Mehr, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi wa Wanafunzi na Wanazuoni wa Hawza ya Qom, aliwasilisha ripoti kuhusu mipango, shughuli na masuala ya majlisi hiyo.
Maoni yako